Unachopaswa Kufanya Tetemeko la Ardhi litokeapo Sehemu ya Mjini
Umeshawahi kufikiria jinsi ya kujilinda ukumbanapo na tetemeko kubwa la ardhi unapokuwa mbali na nyumbani kwako? Bobby, mzawa wa Marekani anatembelea Kituo Kinachotoa Mafunzo ya Kupata Tajiriba ya Kuzuia Majanga cha "SONA AREA TOKYO." "Anashuhudia" uhamaji katika mji mkubwa uliokumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.3 kwenye kipimo cha Richter na kupata vidokezo vya kujiokoa saa 72 za kwanza. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 6, 2021.)
Kituo hicho kina modeli ya majengo makubwa yaliyoporomoka kufuatia tetemeko huku athari za sauti na mwanga zikitoa mioto na wimbi la mitetemo. Wageni wanaweza kupata hisia kamili ya kinachohitajika ili kuhama kutoka eneo la janga.
Katika "Ziara ya Saa 72 ya Tetemeko la Ardhi jijini Tokyo," washiriki wanaelekea eneo la uhamaji wakati wakitumia tableti kujibu maswali yanayohusu hatari na hadhari husika.
Naibu Mkurugenzi wa SONA AREA TOKYO, Sawa Yoshihiro (kulia) anasema mamlaka nchini Japani huwataka wafanyakazi katika miji mikubwa kusalia mahali pao pa kazi kwa siku tatu ikiwa patatokea tetemeko kubwa la ardhi.