Uhamaji
Utahamaje wakati wa mafuriko makubwa yasiyowahi kutokea na tetemeko kubwa la ardhi? Mandy, anayetokea Uhispania, anazunguka mjini akiandamana na Hori Itaru, mtaalam wa kuzuia majanga, na kupata vidokezo vya namna ya kuhama salama na ni nini unachopaswa kujihadhari nacho unapohamia eneo salama. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 4, 2021.)
Bustani hii, iliyotengwa kama makazi ya muda, ina bomba la maji la kutumiwa wakati wa majanga.
Wakati wa mafuriko na maporomoko ya matope, Japani hutumia hadhari ya viwango vitano, vikianzia alama moja hadi tano.
Hakikisha unapitia njia salama unapohama baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi. Usikaribie jengo ambalo ukuta wake wote ulijengwa kwa kutumia gilasi kwani unaweza ukajeruhiwa na gilasi zilizovunjika.
Stuli inaweza ikageuzwa haraka kuwa choo wakati wa janga.