Ramani za Maeneo Yaliyo Hatarini
Japani hukumbwa na majanga ya asili mara kwa mara, lakini wageni wanaofika nchini humo wana tajiriba ndogo sana ya majanga kama hayo. Unafahamu ni majanga ya aina gani asilia yanayoweza kutokea eneo unakoishi au unalotembelea? Ikitokea dharura, wapi na namna gani utahama eneo hilo? Katika kipindi hiki, tunaziangazia ramani za maeneo yaliyo hatarini, zinazoonesha maeneo yanayoweza kuathiriwa na majanga ya asili.
Serikali nyingi za manispaa Japani hutoa ramani hizi kwa lugha za Kiingereza, Kichina na lugha zingine.
Hori Itaru, mtaalam wa hatua za kukabiliana na majanga (kushoto) na Mandy aliyefika Japani kutoka Uhispania miaka mitatu iliyopita (kulia).
Ramani hizi zenye rekodi ya majivu yaliyotiririka wakati Mlima Fuji ulipolipuka karibu miaka 300 iliyopita zina taarifa muhimu kwa ajili ya hatua za kujiandaa kwa majanga ya sasa.
Hori na Mandy walizunguka kata ya Edogawa jijini Tokyo, wakiangalia ramani iliyochapishwa na serikali ya kata ikionesha maeneo yaliyo hatarini ya kukumbwa na mafuriko. Kihistoria, eneo hili limeharibiwa na mafuriko mara nyingi.