Taarifa inaokoa maisha
Pale janga linapotokea, taarifa ambayo ipo wazi, sahihi na inayotolewa kwa haraka ni muhimu. Wakazi wa kigeni nchini Japani, hata hivyo, mara nyingi wanakumbana na matatizo kutokana na matatizo ya lugha na mawasiliano. Utafiti wa jamii moja ya raia wa Brazil wanaoishi Japani waliokumbwa na mafuriko unatoa mwanga kuhusiana na changamoto zinazowakabili na suluhisho linalohitajika. (Kipindi hiki kilitangazwa Aprili 1, 2020.)
Mwezi Septemba 2015, mji wa Joso mkoani Ibaraki ulikumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga.
Escola Opção ni shule ya Kibrazil katika mji wa Joso. Watoto husoma kwa lugha ya Kireno.
Mkuu wa shule Uemura Mayumi
Uemura amekuwa akishiriki katika mabadilishano na raia wa Kijapani katika mji wa Joso.