Umahiri wa Kukabiliana na Taka

WHAT'S YOUR CONNECTION?

dk10 sek00
Siku ya kutangaza Agosti 24, 2019 Inapatikana hadi Agosti 24, 2021

Arthur Kabugu Mathenge husikisiliza matangazo yetu ya Kiswahili na alituambia kuwa, nchini Kenya, taka zote hurundikwa mahali pamoja bila kuchambuliwa, na kusababisha matatizo ya kimazingira. Anataka kujua jinsi Japani inavyokabiliana na taka. Mtangazaji wetu Mkenya wa Idhaa ya Kiswahili Martin Mwanje anazuru Yokohama anakobainisha kuwa wawakilishi kutoka Afrika wametembelea serikali ya mji huo kujifunza jinsi Japani inavyoshughulikia taka. Martin anaripoti kuhusu mtambo wa kushughulikia taka, mbinu za kuchakata na kuchoma taka, na shughuli za elimu zinazowalenga watoto. Pia anazuru mji wa Kamikatsu Mkoani Tokushima usiokuwa na mtambo mkubwa wa kushughulikia taka, lakini umefikia asilimia 80 ya uchakataji taka. Nini siri yake?

Muhtasari wa Vipindi