audio
Kujiandaa na majanga kwa watu wa tamaduni tofauti
WHAT'S YOUR CONNECTION?
dk11 sek34

Siku ya kutangaza Juni 18, 2020
Inapatikana hadi Juni 18, 2021

Tunajifunzaje kuhusiana na kujiandaa na majanga nchini Japani? Katika kipindi hiki watu kutoka Myanmar wanaoishi Tokyo wametutumia swali, ambalo Khin Aye Nge wa idhaa ya Kibama ya NHK WORLD-JAPAN anajaribu kuyajibu. Kwanza, Khin anatembelea nyumba kubwa ya utawa ambapo watu kutoka Myanmar wanaoishi Japani hukusanyika. Sambamba na hao, anakwenda kwenye kituo ambacho wageni wanaweza kujifunza kuhusiana na kujiandaa na majanga na kushiriki katika mifano halisi ya tetemeko la ardhi. Ni kitu gani wanajifunza katika kituo hicho? Kundi hilo pia linapata kukutana na mtaalam wa jumba hilo kubwa la utawa wa kujiandaa dhidi ya tetemeko la ardhi ama moto. Ni matatizo gani wanayapata na ushauri gani wanaupata? (Kipindi hiki kilitangazwa Aprili 2, 2020.)

photo Mhadhara kuhusiana na kujiandaa na majanga kwa watu kutoka Myanmar katika jumba kubwa la utawa la Kibuddha jijini Tokyo. photo Tajiriba ya watu katika tetemeko la ardhi la bandia. photo Mazoezi ya kutumia kizimia moto. photo Washiriki wakifurahia tajiriba