audio
Kanpyo
Vinono kutoka jijini Tokyo
dk11 sek49

Siku ya kutangaza Aprili 29, 2021
Inapatikana hadi Aprili 29, 2022

Kipindi cha "Vinono kutoka jijini Tokyo" kinaangazia vyakula mbalimbali vinavyopatikana kwenye masoko ya jiji hilo ikiwa pamoja na soko la Toyosu. Wakati huu tunaangazia kanpyo, chakula kilichochakatwa kilichovumbuliwa Japani. Kina mwonekano wa tambi nyeupe za nudo zilizo bapa na huchemshwa pamoja na sosi ya soya na sukari ili kutumika katika miviringisho ya sushi. Tunakujuza mhimili uliojificha wa chakula cha Kijapani, kanpyo. (Kipindi hiki kilitangazwa 5 Agosti, 2020.)

photo Wakulima huleta vibuyu ndani na kuvining'iniza kwenye fito ili vikauke. photo Ripota wa NHK WORLD-JAPAN Saskia Thoelen amtembelea muuzaji wa jumla wa vyakula vilivyokaushwa. photo Kibuyu kinachongwa hadi unene wa milimita tatu ili kutengeneza kanpyo. photo Nyama choma ya tochigi yenye kanpyo na vipande vya kitunguu.