audio
Mwanamke Mvietnamu Anayefanya Kazi Kuendeleza Jiji la Tokyo
Kazini nchini Japani
dk10 sek48

Siku ya kutangaza Oktoba 28, 2020
Inapatikana hadi Novemba 11, 2021

Tunakutana na mwanamke mzawa wa Vietnamu anayefanya kazi kuleta maendeleo mapya katika Kata ya Shibuya jijini Tokyo. Kipindi cha Kazini Nchini Japani kinakuwezesha kufahamu maisha ya watu kutoka kote duniani walioichagua Japani kama mahali pao pa kazi. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 14,2020.)

photo Kampuni ambayo Doan Le Hai Ngoc anaifanyia kazi ni moja ya vinara katika ustawi wa miji Japani. Shibuya palipo ofisi yake, kwa sasa ina mradi mkubwa unaoendelezwa upya. photo Doan anaongoza mkutano. Anajihusisha na mradi wa kujenga kituo kipya cha habari za kitalii mbele ya Kituo cha Shibuya. photo Doan akiwa na mkuu wa timu yake. Anampa Doan majukumu ya kumkuna kichwa zaidi kimakusudi. photo Doan akionesha skrini kubwa ya kidijitali iliyojengwa mwaka 2018. Doan na timu yake wanasimamia operesheni na maudhui ya vinavyooneshwa kwenye skrini hiyo.