audio
Kuitambulisha Sake Duniani
Kazini nchini Japani
dk09 sek31

Siku ya kutangaza Machi 31, 2021
Inapatikana hadi Machi 31, 2022

Kipindi cha Kazini nchini Japani kinamulika maisha ya raia wa kigeni wanaofanya kazi Japani. Katika kipindi hiki cha leo, tunatembelea mji wa Tamba mkoani Hyogo magharibi mwa Japani ili kuangazia jitihada za kila siku za Kelley Kaminsky, mwanamke Mmarekani anayevutiwa na utengenezaji wa pombe ya sake. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 15, 2020.)

photo Kelley Kaminsky anafanya kazi katika kiwanda cha sake mjini Tamba, mkoani Hyogo. photo Kelley (kushoto) anataka kuitambulisha sake kwa watu duniani kote; Mkuu wa kiwanda, Yashima Korei (kulia)anayesimamia utengenezaji wa sake. photo Kelley anawathamini sana wafanyakazi wenziwe katika kiwanda hicho.