audio
Kushinda Virusi vya Korona: Ufilipino
Bega kwa bega
dk14 sek19

Siku ya kutangaza Oktoba 29, 2020
Inapatikana hadi Novemba 12, 2021

Virusi vya korona vimekuwa mwiba duniani kote. Vinaathiri maisha ya watu, na baadhi yao wanahangaika kupata chakula cha kila siku kwani wamekuwa wakitatizika kupata pesa tangu kabla ya janga hilo. Nchini Ufilipino, shirika lisilokuwa la serikali la Japani linaendelea na shughuli zake za kuzisaidia familia maskini, likikabiliana na hatari ya maambukizi. Tunampigia darubini Mjapani mmoja na wafanyakazi wake wanaowasilisha misaada kwa wanaoihitaji huku kukiwa na vizuizi mbalimbali. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 15, 2020.)

photo Mtandao ujulikanao kama International Children's Action Network, ICAN wenye makazi yake Japani unaendelea kuwasilisha misaada kwa familia za mapato ya chini huku kukiwa na korona. photo Fukuta Hiroyuki ni mkuu wa tawi la ICAN nchini Ufilipino. photo Mfanyakazi Mfilipino Mariditha Mondares hushiriki shughuli za ICAN huku akifanya kazi kama nesi.