audio
Osaka: Mji wenye Majengo ya Kuvutia
Talii nchini Japani
dk12 sek11

Siku ya kutangaza Aprili 22, 2021
Inapatikana hadi Aprili 22, 2022

Osaka, mji mkubwa ulio magharibi mwa Japani, ni hazina kubwa ya majengo ya aina yake, kuanzia kasri la Osaka, ngome iliyojengwa na jenerali mashuhuri wa karne ya 16, Toyotomi Hideyoshi. Majengo yaliyobuniwa kwa namna ya kuvutia pia yamekuwepo tangu enzi ya Dai-Osaka - yaani Osaka Kuu - mwanzoni mwa karne ya 20, wakati Osaka ulikuwa mji wenye watu wengi zaidi nchini Japani. Kisha, mwaka 1970, mji huo ukawa mwenyeji wa Maonyesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Kibiashara, tukio linalokumbukwa bado kwa Mnara wa Jua. Msanifu majengo kutoka Marekani James Lambiasi, anabaini historia na utamaduni wa Osaka kupitia majengo yake. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 14, 2021.)

photo Msanifu majengo James Lambiasi. photo "Kasri la Osaka" Jengo la kwanza kabisa lilijengwa kuelekea mwishoni mwa karne ya 16, lakini liliungua. Kasri lililopo leo hii lilijengwa tena miaka ya 1930. photo "Mnara wa Jua" ulitengenezwa na msanii Okamoto Taro, mnara huu ulijengwa kwa ajili ya maonyesho ya kibiashara duniani ya mwaka 1970, kama sehemu ya Banda la Maonyesho. photo "Mnara wa Tsutenkaku" una urefu wa mita 100 ukipatikana katikati ya eneo la burudani la Shinsekai, na ni moja ya alama kuu za Osaka.