audio
Yamaguchi: Mandhari na Simulizi Zake
Talii nchini Japani
dk13 sek28

Siku ya kutangaza Septemba 24, 2020
Inapatikana hadi Oktoba 8, 2021

Mkoa wa Yamaguchi upo magharibi ya mbali ya kisiwa kikuu cha Japani, Honshu. Una mandhari mseto yanayotofautiana na sehemu yoyote ya Japani: mfumo wa mapango ya ardhini yenye stalaktiti na stalagmiti tatanishi; kisiwa kidogo ambapo kijiji kinajivunia kuta za kitamaduni za mawe na plasta; na mengine mengi. Mwigizaji Mmarekani Charles Glover anatembelea Yamaguchi kutazama mandhari hayo ya kupendeza na simulizi kuyahusu. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 10, 2020.)

photo Mwigizaji Charles Glover photo "Akiyoshidai Quasi-National Park" ipo mjini Mine, hifadhi hii ina uwanda wa juu zaidi wenye mawe ya chokaa Japani. Njia kadhaa za kustaajabisha zinapita kwenye mawe hayo. photo "Akiyoshido." Moja ya mapango makubwa ya chokaa nchini Japani yaliyo mita 100 chini ya ardhi ya Akiyoshidai. Yanajulikana kwa kuwa na maumbo mazuri ya miamba kama vile madimbwi 100 ya "Hyakumaizara" yenye "mabamba" yaliyojipanga kama trei. photo "Kisiwa cha Iwaishima." Kisiwa hiki kidogo katika Bahari ya Seto kina mzingo wa kilomita 12 tu. Ni maarufu kwa kuta zake zilizoundwa kutoka kwa safu za mawe zinazobadilishana na plasta nyeupe halisi. Kuta hizi zilijengwa kuzuia majengo yasiathiriwe na pepo kali hasa wakati wa vimbunga.