audio
Shizuoka: Ardhi ya Maajabu ya Chai ya Kijani
Talii nchini Japani
dk12 sek09

Siku ya kutangaza Aprili 1, 2021
Inapatikana hadi Aprili 1, 2022

Shizuoka ni kitovu cha uzalishaji mkubwa wa chai ya kijani nchini Japani. Tofauti na chai zingine za rangi, majani ya chai ya kijani hayachachushwi ila yanavukizwa na kukaushwa. Kuna aina mbalimbali za chai hiyo kulingana na mbinu za ulimaji na uchakataji. Mwigizaji Mmarekani Ananda Jacobs anatembelea Shizuoka wakati wa msimu wa mavuno ili kukutana na watu waliojitolea maisha yao kuzalisha kinywaji hicho kizuri. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 16, 2020.)

photo Mwigizaji Ananda Jacobs photo Chai ya kijani ya Kijapani photo Mashamba ya chai katika uwanda wa Makinohara yana ukubwa wa hekta 5,000 na huzalisha 40% ya chai ya kijani ya Shizuoka. Eneo hili la mashamba zamani halikutumika, hadi karibu miaka 150 iliyopita. photo Tochizawa ipo eneo la milimani, upande wa juu kuna mto Warashina. Topografia na hali ya hewa inasababisha hali ya ukungu, unaozuia mwanga wa jua kali, na kufanya kuwa sehemu nzuri kwa uzalishaji wa chai ya ubora wa hali ya juu. Katika eneo hilo mavuno hufanyika kwa mikono, njia ya kitamaduni.