audio
Kufungua Maajabu ya Asuka la kale
Talii nchini Japani
dk11 sek42

Siku ya kutangaza Februari 25, 2021
Inapatikana hadi Februari 25, 2022

Asuka mkoani Nara ilikuwa kituo cha siasa na utamaduni cha Japani kwa miaka zaidi ya 100 kutoka mwishoni mwa karne ya 6. Ustaarabu wa hali ya juu ambao uliendelea huko uliacha kumbukumbu nyingi, hasa maajabu yake ya majengo ya mawe. Kumbukumbu nyingi zimeleta nadharia lukuki. Mwigizaji Luke Bridgford anaangazia mawe haya yaliyowekwa, pamoja na kupitia mafumbo yake na kutembelea maeneo mengine ya kihistoria. (Kipindi hiki kilitangazwa Machi 31, 2020.)

photo Mwigizaji Luke Bridgford photo "Hekalu la Asukadera" lilijengwa mwishoni mwa karne ya 6, lilikuwa hekalu la kwanza la Kibuddha la Japani. Sanamu ya Kibuddha yenye urefu wa takribani mita 3-- moja ya sanamu za kale za Japani--inahifadhiwa kama chombo kikuu cha kuabudia. photo "Ishibutai Kofun Tumulus" Jiwe hili la kaburi pengine la mtu mashuhuri, lilijengwa mwanzoni mwa karne ya 7. Uzito wa jumla wa jiwe hili kubwa unakadiriwa kuzidi tani 2,000. photo "Masudanoiwafune (Meli ya jiwe ya Masuda)" Ilichongwa kutokana na mwamba mmoja, inaaminika kuwa na uzito wa tani 100 kadhaa.