audio
Cherehani Zinazokata Uzi Zenyewe
Uvumbuzi kutoka Japani
dk11 sek40

Siku ya kutangaza Aprili 14, 2021
Inapatikana hadi Aprili 14, 2022

Simulizi zinazoelezea bayana bidhaa maarufu na uvumbuzi kutoka Japani: hiki ni kipindi cha Uvumbuzi kutoka Japani. Wakati huu, tunaiangazia bidhaa inayotumika na kupendwa katika viwanda vya nguo kote duniani: cherehani zinazokata uzi zenyewe. Kanyaga tu pedali kwa mguu, na nyuzi zilizoambatanishwa kwa vipande vya nguo zinakatwa moja kwa moja. Kutoka nembo za hali ya juu hadi mitindo ya kisasa, cherehani hizi zinatumiwa na washonaji kote duniani. Wakati huu, tunazamia katika simulizi isiyojulikana na wengi juu ya uvumbuzi wa cherehani hizo. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 6, 2019.)

photo Cherehani ya kwanza inayokata uzi yenyewe, ilitengenezwa mwaka 1969. photo Shinomiya Hiroaki, mwanachama wa timu iliyovumbua cherehani hiyo. photo Aina mpya ya sasa ya cherehani hiyo.