audio
Mji wa Maebashi Wakutana na Sudan Kusini
Simulizi za Wenyeji
dk12 sek26

Siku ya kutangaza Novemba 26, 2020
Inapatikana hadi Desemba 10, 2021

Wanariadha kutoka Sudan Kusini wamekuwa wakifanya mazoezi katika mji wa Maebashi mkoani Gunma tangu Novemba 2019 ili kujiandaa kwa Mashindano ya Olimpiki na Paralimpiki. Kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu nchini Sudani Kusini, kumekuwa na uhaba wa viwanja vya mazoezi nchini humo. Mji wa Maebashi umejifunga kibwebwe na kuwa mwenyeji wa wanariadha hao. Mji huo umeanzisha mfuko wa kuwasaidia wanariadha hao kuishi kwenye kambi ya mazoezi kwa muda mrefu na kukusanya michango mtandaoni kutoka kote Japani. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 12, 2020.)

photo Timu ya watu watano kutoka Sudan Kusini walisalia Japani mashindano ya Olimpiki yalipoahirishwa, na kambi yao ya mazoezi ya aina yake imeongezewa muda kwa sasa kuendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja. photo Timu hiyo inaongozwa na Guem Abraham Majok Matet anayekimbia mbio za wanaume za mita 1,500. Abraham alifika Japani, akiwa na matumaini makubwa ya mashindano ya Olimpiki kama tamasha la amani. photo Wanariadha hao wamekuwa na fursa nyingi za kukutana na wenyeji wao. Mikutano yao imetoa nafasi kwa watu wa Maebashi kufikiria maswala ya amani. photo Yeni milioni 20 zilichangwa kutoka kote Japani ili kufadhili nyongeza ya muda wa wanariadha hao kufanya mazoezi kambini, na mashirika fadhili pia yalichangia.