audio
Wanandoa, Mji Wao na Gazeti Lake
Simulizi za miji ya nyumbani
dk09 sek28

Siku ya kutangaza Oktoba 20, 2020
Inapatikana hadi Novemba 3, 2021

Mji wa Yawatahama mkoani Ehime, ni mji wa bandari wenye watu 35,000. Mji huo una gazeti lake liitwalo "Yawatahama Shimbun." Lilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1926 na limeendelea kuchapishwa kwa karibu karne moja. Kizazi cha sasa kinachochapisha gazeti hilo ni wanandoa: Matsui Kazuhiro mwenye umri wa miaka 59 na Junko, mwenye umri wa miaka 60. Wakazi wa mji huo walipenda sana makala ya gazeti hilo, lakini wanandoa hao wameamua kulifunga gazeti hilo. Kipindi hiki kinafuatilia safari yao ya mwezi mmoja ya siku za mwisho za kampuni ndogo ya gazeti hilo. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 6, 2020.)

photo Toleo la mwisho la gazeti la Yawatahama Shimbun lililochapishwa mjini Yawatahama kwa miaka 94. photo Matsui Kazuhiro na Junko wanaochapisha gazeti hilo. photo Kazuhiro anayeandika makala yote katika gazeti hilo ameangazia zaidi ufufuaji wa eneo hilo.