audio
Michoro ya Bomu la Atomiki - Hiroshima
Simulizi za miji ya nyumbani
dk12 sek32

Siku ya kutangaza Septemba 15, 2020
Inapatikana hadi Septemba 29, 2021

Simulizi kuhusu watu. Simulizi kuhusu maisha. Kipindi cha Simulizi za Miji ya Nyumbani kinakupa taswira za karibu za watu kutoka kote Japani. Mwako angavu unazunguka hadi juu kwenye mbingu. Maiti iliyotelekezwa barabarani. Picha hizo za kutisha zinatokana na walichokishuhudia manusura wa shambulio la bomu la atomiki la Hiroshima Agosti 6, mwaka 1945. Kwa zaidi ya mwongo mmoja, manusura hao, ama "hibakusha," wamekuwa wakifanya kazi na wanafunzi wa shule ya sekondari ya juu ya eneo hilo kunakili kumbukumbu zao kwenye turubai la michoro. Michoro 137 ya "bomu la atomiki" iliyokamilishwa hadi sasa ni kumbukumbu ya thamani inayoonekana ya maumivu ya kimwili na kihisia yaliyotokana na bomu hilo. Michoro hiyo imesaidia baadhi ya hibakusha kukabiliana na makovu machungu ya kihisia. Na wamekuwa rasilimali bora ya kurithisha ukweli wa siku hiyo. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 1, 2020).

photo photo Hibakusha wanasimulia tajiriba zao za bomu la atomiki kwa wanafunzi wa sekondari ya juu, wanaonakili kumbukumbu hizo kwenye michoro. photo Kwa wanafunzi, kusawiri kumbukumbu za hibakusha ni mchakato wa kusimulia tena tajiriba yao.