audio
Maua Yatachanua Kila Pembe ya Dunia
Tamaduni anuai
dk19 sek21

Siku ya kutangaza Machi 25, 2021
Inapatikana hadi Machi 25, 2022

Baada ya Tetemeko Kubwa la Japani Mashariki la 2011, wimbo wa "Maua Yatachanua" ulitayarishwa kuwafariji waathiriwa wa janga hilo. Sasa, miaka 10 baadaye, wimbo huo umetayarishwa tena katika lugha 11ukiimbwa na wasanii kama May J., Ono Lisa, na Morisaki Win waliojitolea kuimba. Ungana nasi wakati tunapofahamu kilichosababisha kutungwa kwa wimbo huo na kutazama eneo lililoathiriwa na janga hilo kwa sasa. (Kipindi hiki kilitangazwa Machi 11, 2021.)

photo Wasanii 11walioshiriki mradi wa wimbo wa "Maua Yatachanua." photo Mwanamke Mchina anayeishi Minamisanriku atembelea jengo lililobomoka. photo Picha za maua zilizotumwa kutoka duniani kote.