audio
Duka Dogo la Kinijeria la Chris
Tunapopaita nyumbani
dk11 sek11

Siku ya kutangaza Aprili 20, 2021
Inapatikana hadi Aprili 20, 2022

Kaskazini ya Tokyo, kuna mji wa Koshigaya mkoani Saitama. Zaidi ya Wanijeria 500 wanaishi mjini humo kwa sasa. Chris Andrews, anaendesha duka dogo, linalojumuisha duka la jumla na mgahawa unaoihudumia jamii ya Nijeria. Tunafuatilia mahangaiko ya Chris ya kudumisha biashara yake. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 12, 2021.)

photo Chris Andrews alizaliwa nchini Nijeria mwaka 1969. Akiwa na umri wa miaka 27, alikuja nchini Japani. photo Kwenye ghorofa ya pili ya jengo moja, kuna kanisa linakofanyia ibada ya Jumapili kundi moja la Wanijeria. Wengi wa Wanijeria wanafanya kazi viwandani na katika maeneo ya ujenzi mkoani Saitama. photo Imekuwa miaka 25 tangu Chris aondoke nchini Nijeria. Amesaidiwa na marafikize Wajapani. Akikabiliwa na matatizo, upendo wake kwa Japani unaongezeka hata zaidi.