audio
Sehemu ya Kifahari kwa Kila Mtu Kuishi
Tunapopaita nyumbani
dk11 sek03

Siku ya kutangaza Desemba 22, 2020
Inapatikana hadi Aprili 6, 2022

Tumezuru kata ya Shinjuku jijini Tokyo, wanakoishi raia wengi wa kigeni. Mchina Dong Xiaoliang anafanya kazi kwa bidii kusaidia kuwaunganisha wenyenyumba Wajapani na wapangaji raia wa kigeni. Hebu tuangalie kwa karibu juhudi za Dong za kuwatafutia raia wa kigeni pahali pa kuishi wanapoweza kupaita nyumbani nchini Japani. (Kipindi hiki kilitangazwa Desemba 8, 2020.)

photo Dong Xiaoliang ambaye ameishi Japani kwa karibu miaka 20 anaongoza kampuni iliyobobea katika udalali wa nyumba kwa raia wa kigeni. photo Idara ya "Usaidizi wa Kimaisha" hutoa ushauri kwa raia wa kigeni katika lugha zao. Kwa gharama ambayo ni kama asilimia 10 hadi 20 ya kodi zao, wateja wanaweza kutumia huduma hii pamoja na huduma za mdhamini. photo Dong anaishi na mkewe, Ai, kutoka Korea Kusini. Nyumba wanayoishi kwa Dong ni sehemu muhimu wanayoweza kuhisi utulivu. Nyumbani ni msingi wa maisha ya kila siku. Hiki ndicho Dong anachokiamini zaidi.