audio
Chuo Kikuu Kinachokuza Mabadilishano na Utofauti: Rais wa Chuo Kikuu cha Kyoto Seika, Oussouby Sacko
Tunapopaita nyumbani
dk10 sek37

Siku ya kutangaza Oktoba 27, 2020
Inapatikana hadi Novemba 10, 2021

Tunamwangazia Oussouby Sacko, rais wa kwanza wa chuo kikuu nchini Japani kutoka nchi ya Afrika. Amekuwa akijitolea kukuza mabadilishano kati ya wanafunzi Wajapani na wale kutoka ng'ambo ambao idadi yao imekuwa ikiongezeka kutokana na juhudi zake. Hata hivyo, janga la korona linafanya iwe vigumu kwa Sacko kufuatilia ndoto yake ya chuo kikuu kilichofungua milango yake kwa utofauti. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 13, 2020.)

photo Mwaka 2018, Sacko ambaye ni mzawa wa Mali alishindana na maprofesa wawili Wajapani kwa wadhifa wa urais, na alichaguliwa. photo Sacko alikuja Japani mwaka 1991 na kusomea shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Kyoto akitafiti usanifu wa maeneo uliochochea mabadiishano kati ya watu. photo Sacko anaamini hakuna kitu kinachoweza kufikia kile tunachojifunza kutokana na tajiriba ya moja kwa moja. Ni kitu alichojifunza kwa kutangamana na wanafunzi.