audio
Jitihada za Kuhifadhi Shamba la Eneo ~ mkoani Oita, Paul Christie ~
Tunapopaita nyumbani
dk11 sek24

Siku ya kutangaza Septemba 22, 2020
Inapatikana hadi Oktoba 6, 2021

Idadi ya watu waliochagua Japani kuwa makazi yao mapya iliweka historia mwaka 2019, ikizidi watu milioni 2.8. Wanachangia mambo mapya kwa nchi, lakini raia wengi wa kigeni wanahangaika kuendana na jamii hiyo. Kipindi hiki kinaangazia changamoto za raia wa kigeni katika sekta ya utalii akijaribu kukabiliana na athari za janga la korona. Tuliandamana na raia huyo Mwingereza anayeratibu ziara za mashambani mkoani Oita huku akifanya juhudi za kuhifadhi mashamba ya eneo hilo. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 8, 2020.)

photo Paul Christie na familia yake. Paul anaendesha kampuni ya wakala wa safari mkoani Oita. photo Mwanamke akimshukuru Paul kwa kumsaidia kupanda mpunga. photo Paul akipanda mpunga kwenye shamba lililotelekezwa.