audio
Kupambana ili Kurejesha Hali ya Kawaida katika Sekta ya Migahawa
Tunapopaita nyumbani
dk11 sek33

Siku ya kutangaza Agosti 25, 2020
Inapatikana hadi Septemba 8, 2021

Kwa sasa, raia wa kigeni wapatao milioni 2.8 ni wakazi rasmi wa Japani, ambao ni sawa na karibu 2% ya idadi ya watu wote nchini humo. Kipindi hiki cha "Tunapopaita Nyumbani," kinamulika maisha na changamoto wanazozikabili katika jamii ya Kijapani. Wakati huu, tumemwangazia binti mmiliki wa mgahawa, Aya Wu kutoka China anayepambana kudumisha biashara yake wakati wa janga la virusi vya korona. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 11, 2020.)

photo Aya Wu kutoka China anaendesha mgahawa maarufu wa Kichina katika mji wa Kawaguchi, mkoani Saitama. photo Chakula cha pilipili cha mtindo wa Sichuan ni miongoni mwa vyakula pendwa kwa wateja wa mgahawa wake Aya. photo Aya alijitolea kufanya usafi kwenye mtaa wa eneo lake miaka mitatu iliyopita. photo Katika harakati za kufufua mgahawa wake, Aya anajaribu huduma mpya kama vile kuwasilisha chakula kwa wateja.