audio
Wanafunzi wa Kigeni - Mustakabali wa Japani
Mambo Leo
dk10 sek15

Siku ya kutangaza Desemba 24, 2020
Inapatikana hadi Aprili 8, 2022

Zaidi ya wanafunzi 300,000 wa kigeni kwa sasa wanasoma nchini Japani. Baadhi yao wanasaka ajira baada ya kuhitimu. Hata hivyo, wanaathiriwa mno na janga la virusi vya korona. Kipindi hiki kinaangazia wanafunzi wa kigeni nchini Japani wanaohangaika kutafuta fursa, ijapokuwa maisha yao yamebadilishwa kabisa na janga hilo. (Kipindi hiki kilitangazwa Desemba 10, 2020.)

photo Mlipuko wa virusi vya korona umebadilisha kabisa maisha ya Taweesak. photo Wanafunzi wa kigeni wanajifunza Kijapani shuleni kwa "namna mpya". photo Nakamura anawafanyisha wanafunzi wa kigeni mahojiano ya majaribio ili kuwasaidia kufuatia ombi kutoka shule ya lugha ya Kijapani. photo Mwanafunzi huyu wa zamani kutoka Vietnam kwa sasa anafanya kazi katika kampuni moja ya Kijapani.