audio
Kuvuka Mipaka ili Kuokoa Sanaa Maarufu ya Bomu la Atomiki
Mambo Leo
dk15 sek30

Siku ya kutangaza Agosti 20, 2020
Inapatikana hadi Agosti 20, 2021

Agosti 1945, mabomu ya atomiki yalidondoshwa Hiroshima na Nagasaki na kuua mamia ya maelfu ya watu. Maruki Iri, mchoraji mzawa wa Hiroshima na mkewe Maruki Toshi walishuhudia madhara makubwa na kutumia zaidi ya miaka 30 kutengeneza mfululizo wa michoro iliyofahamika kama "Paneli za Hiroshima." Michoro hiyo imekuwa ikionyeshwa katika zaidi ya maeneo 20 duniani kote, ikiwafunza watu kuhusu madhara ya vita. Hata hivyo, paneli hizo zinakabiliwa na hatari ya kuharibika, kwani makumbusho binafsi zinakoonyeshwa yanazeeka. Idadi ya watalii pia imepungua kutokana na janga la korona. Ni hatua gani zinachukuliwa kuhifadhi kazi hizo za thamani za sanaa kwa ajili ya vizazi vijavyo? (Kipindi hiki kilitangazwa 06 Agosti, 2020.)

photo Sehemu ya mfululizo wa michoro 15 inayosawiri madhara ya shambulio la bomu la atomiki, "Paneli za Hiroshima." photo Makumbusho ya Maruki yalifunguliwa mkoani Saitama mwaka 1967 ili kuonyesha paneli hizo wakati wote. photo Maruki Iri na mkewe Maruki Toshi kwa pamoja walitengeneza "Paneli za Hiroshima."