audio
Uendelezaji tena mkubwa wa Shibuya-Je Majengo marefu na Miji ya zamani inaweza kuwa pamoja?
Mambo Leo
dk12 sek06

Siku ya kutangaza Juni 3, 2020
Inapatikana hadi Juni 3, 2021

Eneo la Shibuya jijini Tokyo linapitia uendelezaji tena mara moja baada ya karne moja. Majengo marefu kupita kiasi yanajitokeza kaibu na stesheni ya Shibuya moja baada ya jingine, na kusababisha mabadiliko makubwa katika eneo la mjini. Mtangazaji wa idhaa ya Kirusi, Anastasia Monakova, ambaye anasema pia anavutiwa na mandhari ya kitamaduni ya Shibuya, anaripoti juu ya  mradi huo mkubwa wa endelezaji ili kufahamu iwapo mandhari ya nyuma itahifadhiwa. (Kipindi hiki kilitangazwa Machi 19, 2020.)

photo Anastasia Monakova akiripoti katika viwanja vinavyofahamika sana ya "Scramble." Nyuma yake upande wa kulia ni Uwanja wa Scramble Shibuya, jengo la ghorofa 47 lililokamilika Novemba 2019. photo Ushoroba wa ghorofa ya pili unawezesha kupita kati ya majengo marefu. Mara ujenzi utakapokamilika, watu wataweza kupita kati ya majengo hadi kwenye shoroba popote kati ya ghorofa ya pili ya chini ya ardhi na ghorofa ya nne. photo Mtaa wa manunuzi wa Shibuya Center-Gai kwa upande mwingine wa stesheni unaweka tofauti kubwa ya majengo marefu ya siku za baadaye. Upande wa chini kushoto ni ToToshiuki Ono, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kuhamasisha Center-Gai. photo Picha ya viunga vya stesheni ya Shibuya baada ya kukamilika kwa ujenzi mwaka 2027.