audio
Sabuni Iletayo Matumaini
Mambo Leo
dk11 sek10

Siku ya kutangaza Juni 23, 2020
Inapatikana hadi Julai 7, 2021

Sabuni za miche za kufungashwa ambazo unaweza kudhani ni pipi za matunda, kwa sasa ni maarufu. Sabuni hizi zinatengenezwa na watu wenye ulemavu. Katika kiwanda kimoja cha sabuni mjini Odawara mkoani Kanagawa, wafanyakazi 24 wenye ulemavu wa akili, na ulemavu wa viungo wanafanya kazi pamoja. Wanaendelea kufanya shughuli mpya na kupata ujuzi ambao mashine haiwezi kurudufu. Tutakupeleka ndani ya kiwanda hicho kidogo cha sabuni, kilichofanikiwa kibiashara na sehemu ambayo watu hukua pamoja. (Kipindi hiki kilitangazwa Desemba 3, 2019.)

photo Sabuni za miche zenye mwonekano mzuri wa matunda. photo Kila sabuni imetengenezwa kwa mikono na watu wenye ulemavu. photo Kaoru Kambara, Mwenyekiti wa kampuni