audio
Hikikomori Japani Wafunguka Kupitia Mazungumzo
Mambo Leo
dk11 sek21

Siku ya kutangaza Mei 27, 2020
Inapatikana hadi Mei 27, 2021

Nchini Japani, hali ya kukwepa kutangamana na jamii kama kwenda kazini au shuleni na kujifungia nyumbani kwa zaidi ya miezi 6 inafahamika kama "Hikikomori." Zaidi ya watu milioni 1.1 nchini Japani wanakadiriwa kuwa Hikikomori. Kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu sheria dhidi ya hikikomori baada ya vyombo vya habari kuripoti kwamba mshambuliaji aliyewachoma watu visu mnamo Mei 2019 na kusababisha vifo na majeruhi 20 hasa wanafunzi wa shule ya msingi, alikuwa kwenye hali ya Hikikomori. Tunaangazia watu wenye tajiriba ya hikikomori wanaojitahidi kupaza sauti zao na kuhusu tiba ya mazungumzo inavyowasaidia watu hao. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 17, 2019.)

photo Mkutano wa dharura ulifanywa na watu wenye tajiriba ya hikikomori na wanaowaunga mkono photo Profesa Tamaki Saito wa Chuo Kikuu cha Tsukuba, daktari wa magonjwa ya akili amekuwa akiwaunga mkono hikikomori kwa miaka sasa photo Naohiro Kimura, mhariri mkuu wa "Hikikomori Newspaper," ana tajiriba ya kuwa hikikomori