audio
"Kamishibai" Ukumbi wa Picha Unaoeneza Amani
Mambo Leo
dk12 sek41

Siku ya kutangaza Januari 31, 2019
Inapatikana hadi Januari 31, 2020

Wanawake 2 wameanza kutoa wito kwa watu kutokana na janga la mashambulio ya bomu la atomiki na umuhimu wa amani kwa kutumia ukumbi wa picha wa "Kamishibai". Mmoja wa wanawake hao ni Mmarekani ambaye babu yake alikuwa mateka wa vita nchini Japani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Mwingine ni Mjapani ambaye babu yake alikuwa pia amefungwa jela kwa sababu alitabiri na kuonya juu ya nchi yake kushindwa vita.

photo Eiko Matsui, Mjapani aliyeandaa "Never Again" Kamishibai akisisitiza umuhimu wa amani. photo Sydney Solis (kulia), akielekezwa na Eiko Matsui (kushoto) jinsi ya kucheza. photo Sydney alicheza onyesho la Kiingereza la "Never Again" mbele ya hadhira ya Wajapani.