audio
Ramani ya Mustakabali mzuri: Mwalimu wa lugha ya Kijapani Shuji Matsuoka
Ana kwa Ana
dk14 sek32

Siku ya kutangaza Juni 25, 2020
Inapatikana hadi Julai 9, 2021

Cambodia imekuwa na ukuaji mkubwa wa uchumi, lakini manufaa yake hayafurahiwi na eneo hilo zima, na pengo la kiuchumi linazidi kukua. Katika maeneo ya vijijini, watoto wengi wanapoteza hamasa ya kusoma kwa kuwa wazazi wao hawawezi kumudu kununua vitabu vya kiada ama vifaa vya kuandikia kwa ajili yao. Katika hali kama hiyo, Shuji Matsuoka kutoka Japani amekuwa akitengeneza nyenzo za elimu ambazo zinasaidia watoto kujifunza kupitia kucheza, kwa kushirikiana na wenyeji na kuziwasilisha kwa watoto katika shule za msingi bila malipo. Mpango huo wenye juhudi za Mjapani mwenye umri wa miaka 39 unasaidia watoto kupata hamu ya kusoma. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 15, 2020.)

photo Shuji Matsuoka anatoa wito kwa shule za msingi kutoa bure nyenzo za elimu. photo Shuji Matsuoka photo Ramani inaweza pia kutumika kama gemu ya kucheza. Watoto wanazungusha kete kwa kuigeuza na kujaribu kuwa wa kwanza kusafiri nchini Cambodia