audio
Magari ya zimamoto Japani
Uvumbuzi kutoka Japani
dk14 sek05

Siku ya kutangaza Juni 2, 2020
Inapatikana hadi Juni 2, 2021

Pale tetemeko la ardhi la mashariki mwa Japani lilipotokea mwaka 2011, magari ya zimamoto yaliwahi katika maeneo yenye moto kutoka kote nchini Japani ili kutoa msaada unaohitajika. Magari ya zimamoto ya Japani yameendelea kwa kujifunza kutokana na majanga makubwa kama hayo. Kipindi hiki kinaangazia magari ya zimamoto ya hivi leo yaliyosheheni teknolojia ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na lori ambalo linaweza kuzima moto kwa urefu na kuokoa watu katika kiti cha magurudumu. Aina nyingine ya lori la zimamoto lina kifaa ambacho kinazima moto kwa kutumia hewa ya naitrojeni badala ya maji. (Kipindi hiki kilitangazwa Machi 17, 2020.)

photo Kampuni ya kutengeneza vifaa vya zimamoto, lori la Morita photo Ngazi ya lori ambayo inaweza kuzima moto kwa urefu na kuokoa watu katika kiti cha magurudumu. photo Miracle N7 imewekewa mfumo wa hewa yenye naitrojeni ambayo unatoa hewa yenye mkusanyiko wa naitrojeni na kupunguza kiwango cha oksijeni katika eneo ili kuzima moto. photo Mkuu wa idara ya mauzo ya Morita, Mamoru Jougamoto (kushoto) na mtengenezaji Kouichi Yamano (kulia)