audio
Bakuli kubwa lenye michoro ya maua na ndege (Kauri ya Imari, aina ya Kakiemon) (Iroe kachoumon o-fukabachi)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek42

Siku ya kutangaza Februari 6, 2018
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Bakuli lenye muundo wenye rangi za kupendeza za ndege na maua katika rangi nyeupe ya msingi. Ni Kazi ya kauri aina ya Kakiemon ya Imari, jina kivuli lililotumika kuelezea aina mbalimbali za vyombo vya kauri vilivyosafirishwa nje ya Japani kwenda mataifa mbalimbali duniani kutokea bandari ya Imari kati ya karne ya 17 na 18. Utengenezaji wa bidhaa za kauri ulianza nchini Japani wakati utawala wa Hideyoshi ulipovamia Korea na baada ya watengenezaji wa ufinyanzi kutoka Korea walipopelekwa Japani na kugundua uwepo wa kaolini ambayo ni mali ghafi ya kutengenezea kauri katika kisiwa cha Kyushu. Vurugu za mabadiliko ya kiutawala huko China baadaye zilisababisha sekta ya utengenezaji kauri ya Japani kuanza kuibuka. Kwa upande mwingine mbinu za utiaji rangi za enameli za kupendeza ilienezwa wakati watengenezaji wenye ujuzi wa vyombo vya kauri kutoka China walipokimbilia Japani. Pia kwa upande mwingine, usumbufu kama huo ulisababisha usafirishaji wa bidhaa za kauri kutoka China kusitishwa. Wafanyabiashara wa Uholanzi waliokuwa wametawala sekta ya biashara ya bara la Asia kwa wakati huo badala yake wakaanza kusafirisha nje bidhaa za kauri za Japani kwenda mataifa mbalimbali duniani. Bakuli hili la kupendeza tunalotambulisha katika kipindi hiki lilibuniwa zama hizo za mabadiliko makubwa ya kihistoria.

photo