audio
Mti wa Mvinje kazi ya Kano Eitoku (Hinokizu byobu)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek32

Siku ya kutangaza Novemba 9, 2017
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Mchoro wa mti mkubwa wa mvinje una urefu wa mita moja na sentimita 70 na upana wa mita 4 na sentimita 60. Karibu sehemu yote ya nyuma imepambwa kwa foili ya dhahabu, ambayo inaonyesha muonekano wa mti mkubwa. Kazi hii ilichorwa mwishoni mwa karne ya 16 katika kipindi ambacho wababe wa kivita wenye nguvu walikuwa wanajitokeza baada ya miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe huku kukiwa na juhudi za kuunganisha Japani. Kano Eitoku, mbunifu wa kazi hii, ni mchoraji aliyependwa na mamlaka. Alikuwa anarithisha utamaduni wa sanaa ya babu yake, mwanamume ambaye aliunganisha utamaduni wa uchoraji unaotumia wino kutoka China na utamaduni wa zamani wa Japani wa kuchora kwa kutumia rangi zinazopendeza. Kisha akachora picha zinazopendeza ambazo zilipendwa na wababe wa kivita. Hususan kazi hii, ilichorwa kwenye milango ya karatasi inayoteleza katika makazi ya familia ya mfalme lakini baadaye ikabadilishwa na kuwekwa kwenye milango inayokunjika. Kazi nyingi za Eitoku zilipotea kwa sababu ya vita lakini mchoro huu umedumisha kumbukumbu yake.

photo