audio
Daryukyo – Kioo cha shaba nyeusi chenye Mapambo bora na Majitu
Sanaa za Kijapani
dk13 sek31

Siku ya kutangaza Oktoba 12, 2017
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Kazi ambayo tumekufahamisha hii leo ni kioo cha shaba nyeusi kilichotengenezwa karne ya nne. Vioo vilikuwa na nguvu ya kuakisi picha za watu au kuwasha moto na kuchukuliwa kama bidhaa bora wakati wa zamani. Vioo vingi vilivyoingizwa kwenye visiwa vya Japani kutoka China vilikuwa nembo ya mamlaka na vilizikwa kama bidhaa za makaburini kwenye makaburi ya watu waliokuwa na mamlaka. Hususan kioo hiki tunachoangazia, pia kilifukuliwa kutoka kwa tuta la kaburi lakini kilitengenezwa kutoka funguvisiwa vya Japani mfano wa kioo cha China. Kikiwa na kipenyo cha sentimita 44.5, ni kikubwa kwa viwango vya Asia Mashariki na kilikuwa kimetengenezwa kwa utaalamu wa kukalibu. Vioo ambavyo ni chimbuko lake, viliwakilisha dunia ya miungu kama ilivyokuwa inafikiriwa na watu wa China lakini mafundi stadi wa Japani hawakuelewa nembo hizo zinamaanisha nini na badala yake wakavibadilisha hadi mapambo ya kipekee. Hii ni kazi ambayo inaangazia historia ya mabadiliko ya utamaduni eneo la Mashariki mwa Asia wa kale.

photo