audio
Kasha lililotengenezwa kwa mbinu ya Maki-e na kupakwa vanishi lenye ubunifu wa daraja la pantoni linalowekwa vifaa vya kuandikia lililotengenezwa na Hon'ami Koetsu (Funabashi Maki-e Suzuribako)
Sanaa za Kijapani
dk13 sek09

Siku ya kutangaza Julai 13, 2017
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Suzuribako ni kasha la kuwekea vifaa vya kuandikia. Makasha kama hayo pia yalitumika kama mapambo ya vyumbani na kuwa kazi za ufundistadi zinazovutia kwa lengo hili. Kasha hili la mwanzoni mwa karne ya 17 lina muundo wa daraja la pantoni ambalo liko juu ya mfuniko. Umbo lake madhubuti liliwakilisha mwanzo wa mabadiliko makubwa kutoka kwa mbinu ya kitamaduni ya maki-e ambayo tayari ilikuwepo miaka mingi iliyopita iliyojumuisha ungaunga wa madini ya dhahabu na fedha na kupakwa vanishi. Mtengenezaji wa kasha hilo Hon’ami Koetsu, alitoa kazi ya pamoja katika nyanja mbalimbali na mafundistadi na wasanii wengi. Utawala wa Shogun, Tokugawa Ieyasu, ulimpa ardhi viungani mwa Kyoto ambapo alianzisha kijiji cha ufundistadi. Karne moja baadaye, mtu wa familia hiyo hiyo msanii Ogata Korin, alivutiwa kwa kiasi kikubwa na Koetsu akabadili mwelekeo wa historia ya sanaa ya Kijapani.

photo