audio
Kipepeo cha kukunjika kilichotumiwa na makasisi wa kike wa kisiwa cha Amami Oshima (Kamiougi)
Sanaa za Kijapani
dk13 sek37

Siku ya kutangaza Mei 11, 2017
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Kipepeo hiki kina ukubwa wa zaidi ya mita moja. Pande zote mbili zimepambwa upande wa mbele ukionyesha jua na ndege aina ya finiksi wawili, huku upande wa nyuma ukionyesha mwezi na vipepeo na maua. Vyote vimetokea Utawala wa Ryukyu, fungu la visiwa hadi kusini mwa Japani. (Vilichukuliwa na Japani karne ya 19 na kutengeneza Okinawa ya sasa). Kipepeo hicho kilitengenezwa kwenye karakana ya kifalme na ni miongoni mwa zawadi zilizotolewa na Mfalme kwa makasisi wa kike kwa ajili ya hafla za kidini. Katika eneo la Ryukyu, iliaminika kwamba wanawake walilinda waume kutokana na nguvu yao ya kiimani, na mfalme mwenyewe alisaidiwa na malkia. Pia aliongoza shughuli za kidini na kasisi wa kike alipewa jukumu katika kila kisiwa na vijijini kuhudumia miungu. Kipepeo hicho kilikuwa ishara ya jukumu hilo muhimu. Jua liliashiria mfalme huku mwezi ukiwa malkia na kipepeo kilikuwa kitu cha kipekee kikiashiria nguvu ya miungu.

photo