audio
Vazi la kujihami wakati wa mapambano la Domaru lenye lesi ya rangi mbalimbali (nyuzi za rangi nyekundu kwenye mabega)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek46

Siku ya kutangaza Machi 16, 2017
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Domaru ni moja ya mtindo unaowakilisha vazi la Kijpani la kujihami wakati wa mapambano. Kuanza vazi hilo la kujihami lilivaliwa na askari wa kutembea kwa miguu, taratibu likaanza kutumiwa hata na samurai wa ngazi ya juu kabisa. Vazi la domaru linaloangaziwa katika kipindi hiki linaaminika kwamba ilitengenezwa karne ya 15 kwa ajili ya wababe waliotawala kaskazini mwa Japani. Vazi la kujihami wakati wa mapambano la Kijapani lilitengenezwa kwa kuunganisha vipande vingi vya chuma na ngozi kwa kutumia kamba na mapambo ya kipekee ya vazi hilo yakatengenzwa pale ambapo kamba hizo zilijitokeza kwa nje. Kushona mchanganyiko wa rangi ya buluu iliyokolea na nyekundu ilitumika katika sehemu nyingi za vazi la domaru hilo lakini kamba za rangi nyekundu pekee zinatumika kwenye mabega, kifua na sehemu zingine zikawa na muonekano wa kupendeza. Mapambo ya rangi ya dhahabu pia yametengenezwa vizuri kwa kutumia mkono. Vazi la kujihami wakati wa kivita la Kijapani lilikuwa ni muunganisho wa kazi za sanaa zilizotengenezwa na wasanii mbalimbali.

photo