audio
Azekura (Hifadhi ya maandiko ya sutra ya Kibuddha)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek12

Siku ya kutangaza Februari 9, 2017
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Kibanda kidogo cha mraba chenye takribani urefu zaidi kidogo ya mita nne kinapatikana katika bustani ya makumbusho ya Taifa ya Tokyo. Kilijengwa kwa mtindo unaofahamiaka kama azekura wa kukusanya mbao za umbo la pembe tatu ambao ulitumiwa kwa ajili ya nyumba za hazina kuanzia karne ya 8. Kibanda cha azekura kilichopo katika makumbusho ya Taifa ya Tokyo kilijengwa katika karne ya 13 na awali kilikuwa katika hekalu mkoani Nara lakini kikahamishwa kwa ajili ya kujengwa upya katika makumbusho iliyokuwa imekamilika kujengwa jijini Tokyo mwishoni mwa karne ya 19. Huu ni wakati ambapo majengo ya kibuddha na bidhaa zilikuwa zinaharibiwa katika sehemu nyingi za Japani kutokana na sera ya serikali ya kufanya Shinto kuwa dini ya taifa. Hisanari Machida alitoa wito wa kulinda bidhaa za kitamaduni za kale na kuanzisha makumbusho. Alikuwa amejifunza kuhusu jukumu la makumbusho katika nchi za kisasa wakati huo, akiwa ziarani Ulaya na uhifadhi wa bidhaa za kitamaduni za Japani ukaanza chini ya uongozi wake. Kibanda hiki kidogo mtindo wa azekura ni moja ya bidhaa zilizookolewa wakati huo uliokuwa na changamoto.

photo