audio
Simulizi ya Matsuranomiya (Matsuranomiya Monogatari)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek05

Siku ya kutangaza Desemba 8, 2016
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Simulizi ya Matsuranomiya iliandikwa mwishoni mwa karne ya 12 na mkabaila ambaye pia alikuwa msomi wa fasihi, Fujiwara-no-Teika. Ni simulizi ya kijana kabaila wa Kijapani aliyetembelea China na anakumbana na matukio mengi ya kushangaza. Huku matukio yaliyojaa dhana mbalimbali yakijumuishwa kwenye kazi za fasihi za zamani, maelezo ya vita yanaakisi tajriba ya vita ya Teika na kuibuka kwa tabaka la wapiganaji wa Kijapani. Kazi ambayo tumeiangazia hii leo ni nakala ya maandishi iliyotolewa takribani karne moja baada ya enzi za uhai wa Teika. Historia ya Japani ilikuwa imefikia kipindi cha mabadiliko makubwa. Nakala hiyo inaonekana kwamba imetengenezwa kwa lengo la kuwasilisha uliokuwa utamaduni wa kikabaila. Karatasi hizo zilizotumika katika nakala hiyo ya kitabu ambazo ni za kupendeza zilizopambwa zikawa hazipatikani tena. Kwa upande mwingine maandishi hayo ya kipekee huenda yaliandikwa hivyo kwa ajili ya wasomaji wapya ili wapiganaji na wengine waweze kuelewa simulizi pia.

photo