audio
Bakuli lenye mchoro wa ndege kitwitwi (Mino ware, Nezumi Shino type)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek48

Siku ya kutangaza Oktoba 20, 2016
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Bakuli la duara lenye kina kifupi ambalo halikutengenezwa kwa usahihi... Sehemu kubwa ni ya rangi ya kijivu lakini unaweza kuona ndege kitwitwi aliyetulia kwenye mwamba katika mkondo akiwa kwa rangi nyeupe. Mbinu ya kawaida ilikuwa ni kupaka rangi kwanza na kuondoa sehemu za bakuli hilo kupata muundo uliohitajika. Hata hivyo kwa kuzingatia picha hii, sehemu ya udongo ilikuwa ikipuuzwa wakati wa kupaka rangi bila kukusudia. Umbo hilo lilitokea kuonekana kama mwamba na hatimaye kupatikana kwa muundo huu. Mwishoni mwa karne za 16 na 17 nchini Japani ulikuwa ni wakati wa mabadiliko katika jamii kutokana na vita na shughuli za kiuchumi, na hilo likachangia kupatikana kwa mambo mapya ya sanaa. Mtindo huru wa Shino ambao unajitokeza kwenye bakuli hili ulikuwa unawakilishi ufahamu wa mambo hayo mapya ya sanaa katika dunia ya bidhaa za kauri. Hatimaye, hamu ilibadilika tena kiasi kwamba watu walisahau kule ambako kazi hizi zilitengenezwa. Ugunduzi tena wa tanuri za Mino ambako ni chimbuko la kazi zilizotengenezwa kwa kutumia mbinu ya Shino ulianza karne ya 20 na kwa sasa tunafahamu jukumu kubwa lililotekelezwa katika utengenezaji wa bidhaa za kauri za wakati huo .

photo