audio
Kanjo-ban (pambo lililotumika katika ibada za kibudha)
Sanaa za Kijapani
dk16 sek13

Siku ya kutangaza Septemba 15, 2016
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Pambo la ban ni refu, jembamba linalotumika katika hafla za kibuddha. Mapambo kama hayo hupamba mahekalu wakati wa maombi kwa ajili ya kuwakumbuka waliokufa na usalama wa maeneo. Ingawa kawaida huwa vinatengenezwa kwa hariri, Kanjo-ban, pambo ambalo tutaliangazia katika kipindi hiki, lilitengenezwa kwa vipande vidogo vya shaba vyenye mpako wa dhahabu. Hakuna pambo kama hilo ambalo lilitengenezwa katika nusu ya pili ya karne ya saba lilirithishwa kwenye hekalu la Horyuji, moja ya mahekalu ya zamani nchini Japani. Pambo hilo lina urefu wa zaidi ya mita tano na linajumuisha kunakshiwa kwa kuchongwa kukiwakilisha dunia ya imani ya kibuddha na kile kinachoaminika ni malaika wakicheza kwa uhuru angani. Pambo hili la kipekee huenda lilitengenezwa kutokana na agizo la binti wa mwana mfalme Shotoku Taishi, aliyetambuliwa kwa kuanzisha imani ya Kibuddha nchini Japani. Mtunzaji wa makumbusho ya Taifa ya Tokyo Kakuyuki Mita anapendekeza kwamba huenda alifanya hivyo kumkumbuka kakake mkubwa, aliyejiua baada ya kuhusishwa na mzozo wa urithi wa kifalme.

photo