audio
Nuihaku, ni vazi la sanaa ya Noh linalovaliwa na wanaoigiza kama wanawake vijana (Nuihaku, Kohakudan kusabana tanzaku yatsuhashimoyo)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek27

Siku ya kutangaza Julai 14, 2016
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Nuihaku ni aina ya vazi la kimono lenye mapambo yaliyodariziwa pamoja na vipande vya dhahabu na fedha. Vazi la nuihaku tunaloangazia katika makala hii limetengenezwa kwa kitambaa chenye maumbo ya miraba ya rangi nyekundu na nyeupe likiwa na mapambo mbalimabli yaliyodariziwa kama vile maua na miti ya misumu tofauti tofauti. Awali kulikuwa na vipande vya dhahabu na fedha katika nafasi zilizoachana. Vazi hilo la kuvutia linaashiria ubunifu wa mapambo ya kipekee ya mwishoni mwa karne ya 16 na mapema 17 na inaaminika kwamba lilitengenezwa kwa ajili ya mwanamke mwenye hadhi ya juu kabla ya kuanza kutumika kama vazi kwa ajili ya sanaa ya Noh. Sanaa ya kipekee ya Noh ya Japani ilipendwa na wababe wa kivita na hakuna mwengine anayoweza kufananishwa na Toyotomi Hideyoshi, mwanamume aliyeunganisha Japani mwishoni mwa karne ya 16. Hakutawala tu sanaa ya Noh bali pia alichukuwa jukumu na kuwa miongoni mwa waigizaji. Kulingana na yaliyokuwemo katika mapambo ya vazi hilo, inasemekana kwamba huenda chimbuko la vazi hilo la nuihaku ni nyumbani kwa Hideyoshi mwenyewe.

photo