audio
Attushi – Makoti ya kitamaduni ya watu jamii ya Ainu
Sanaa za Kijapani
dk13 sek19

Siku ya kutangaza Juni 9, 2016
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Attushi ni koti la kitamaduni la watu wa asili ya Ainu ambao waliishi kaskazini mwa Japani. Makumbusho ya Taifa ya Tokyo ina mkusanyiko wa attushi za karne ya 19. Kuna wakati ambao watu wa Ainu walifanya biashara katika eneo pana kutoka Hokkaido hadi eneo la Mashariki ya mbali la Urusi na kuwa utamaduni wa kipekee. Attushi, zilizotumiwa katika mavazi ya kawaida na yale ya matukio maalum bado ni ishara kamili ya utamaduni wa watu wa Ainu. Kitambaa kimetengezwa kwa nyuzinyuzi zilizotokana na miti. Kwa maumbo, yanafanana na mavazi ya kimono ya Kijapani lakini kinachovutia zaidi ni maumbo ya Ainu yaliyodariziwa kwa pindo zenye rangi ya buluu iliyokolea. Utengenezaji wa nyuzinyuzi, ufumaji na kudariziwa zilitengenezwa hasa kwa kutumia mikono kazi zilizofanywa na wanawake. Kwa sasa dhamira ya kutunza utamaduni wa watu wa Ainu inaendelea kuwa imara na wanawake bado wanatengeneza attushi kwa namna ya kitamaduni.

photo