audio
Mandhari iliyochorwa kwa wino kazi ya msanii Sesshu (Haboku Sansuizu)
Sanaa za Kijapani
dk16 sek01

Siku ya kutangaza Aprili 14, 2016
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Mandhari iliyochorwa na Sesshu, kwa kutumia wino, anayewakilisha wasanii wa karne ya 15 nchini Japani. Picha za kwenye mchoro huo zinapatikana tu upande wa chini wa mviringisho. Theluthi mbili ya sehemu iliyosalia hivi, ina maandishi. Makasisi sita waliandika mashairi upande wa juu na Sesshu mwenyewe akaandika katika sehemu ya katikati, akielezea tajriba yake ya kusafiri hadi China na kusoma chini ya wachoraji wa picha za kifalme, na fikra zake kwa walimu. Kwa kufuatilia hatua zilizomfanya Sesshu kutoa kazi hii, unagundua enzi ambayo makasisi wa Zen walitekeleza jukumu muhimu la kitamaduni. Sanaa ya uchoraji kwa kutumia wino ilishamiri kwenye mahekalu ya Zen, mahali ambapo maisha ya kila siku yalichukuliwa kuwa matendo ya kidini. Vilevile, Sesshu, ambaye alikuwa kasisi wa Zen na washairi wa mashairi kwenye mviringisho huo, walikuwa makasisi wa ngazi ya juu wakati huo. Kazi hiyo, inathibitisha mabadilishano ya wasomi wa hali ya juu yaliyotokea kati ya makasisi wa Zen wakati huo.

photo