audio
Hyokeikan – Makumbusho ya zamani zaidi ya kazi za sanaa nchini Japani. (Hyokeikan)
Sanaa za Kijapani
dk14 sek28

Siku ya kutangaza Machi 3, 2016
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Kuba ndefu, iliyojengwa mtindo wa kimagahribi iko kiungani mwa makumbusho ya Taifa ya Tokyo. Baada ya ujenzi wake kukamilika mwaka 1908, ilipewa jina la Hyokeikan, yaani jengo linaloonyesha furaha, na ilijengwa kwa ajili ya sherehe ya harusi ya mwana mfalme. Lilisanifiwa kama makumbusho ya sanaa ya kwanza ya Japani iliyojengwa na mmoja wa wasanifu wa kwanza wa majengo wa Kijapani. Japani ilikuwa ikiiga utamaduni na mifumo ya magharibi katika harakati za kuingia kwenye usasa wakati huo, katika nusu ya pili ya karne ya 19 na ilihitaji wataalamu kusanifu majengo kwa mtindo wa kimagharibi. Josiah Conder, msanifu aliyealikwa kutoka uingereza, alifundisha historia na miundo ya usanifu wa kimagharibi kwa wanafunzi wa Kijapani. Darasa lake la kwanza lilijumuisha Tohkuma Katayama, aliyekuwa msanifu wa majengo ya Kifalme na kusanifu jengo la Hyokeikan. Hii ndiyo simulizi ya waanzilishi hao wakati wa muamko wa mtindo wa usanifu wa kimagharibi nchini Japani.

photo