audio
Kipengele cha Koya, mkusanyiko wa mashairi ya zamani na ya kisasa, Mviringisho wa 19 wa karatasi. (Kokin Wakashu "Koyagire")
Sanaa za Kijapani
dk12 sek56

Siku ya kutangaza Januari 21, 2016
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Japani ilifanya mageuzi ya kipekee ya kiutamaduni kutokana na desturi na utamaduni wa China katika karne ya 10 na 11. Kokin Waka Shu – mkusanyiko wa kazi za zamani na mpya za ushairi wa waka – ni mojawapo ya mageuzi yanayowakilisha zama hizo. Namna mwafaka ya kuandika mashairi ya waka ilikuwa ni kutumia herufi za hiragana zilizobuniwa kwa kurahisisha herufi za kichina. Kazi tunayoangazia inatoka kwenye nakala ya karne ya 11 ya Kokin Waka Shu, na inachukuliwa kama kilele cha kaligrafia ya hiragana. Uandikaji wa kutumia brashi yenye ncha nyembamba kwenye karatasi inayong’aa yenye chembechembe za madini ya ulanga, maandishi hayo yameunganika vema kutoka juu kwenda chini kwa mistari kadhaa. Mwandikaji wa kaligrafia hiyo anaaminika alitoka kweye tabaka tawala, na imekuwa msingi wa herufi za hiragana zinazotumika hivi leo nchini Japani. Tunaangazia historia ya zamani ambapo nakala halisi za kuviringisha zilikatwa kwenye vipande vigodovidogo kwa ajili ya kujifurahisha na kuakisi uzuri wa mtindo wa kaligrafia wa kijapani.

photo