audio
Koti (lililovaliwa wakati wa vita, jin-baori), lililoshonwa kwa kutumia uzi mwekundu huku likiwa na muundo wa mundu. (Jin-baori Shojo-hi Rashaji Chigai-kamamon)
Sanaa za Kijapani
dk15 sek39

Siku ya kutangaza Desemba 3, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Japani ilipigana vita vingi vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwishoni mwa nusu ya karne ya 15 hadi karne ya 17. Wapiganaji wa kipindi hicho walishindana miongoni mwao kuvaa bidhaa zilizokuwa za kipekee ambazo zingewafanya kuonekana kwamba ni wa kipekee. Hususan, viongozi wa vita hivyo, walivaa jinbaori – makoti yaliyovaliwa juu ya ngao wakati wa vita– ili kutambulika. Koti la rangi nyekundu lililovaliwa wakati wa vita ambalo tumeliangazia katika kipindi hiki, lina muundo unaoonekana wazi wa mundu upande wa nyuma huku kwa mbele, likionekana kama muundo wa lango la kuingia kenye hekalu ambalo linaashiria matakwa binafsi ya wapiganaji ya kutaka ulinzi kutoka kwa miungu. Kitambaa kilichotengenezwa kwa sufi kilichotoka Ulaya, kilitiwa rangi ambayo ilikuwa ghali na huenda kiliwasili nchini Japani kupitia ufanyaji biashara na wareno. Utumiaji wa vitambaa vyenye thamani kama hivyo pia ulikuwa ishara ya kuonyesha nguvu. Pia utagundua hisia ya kutaka kutambulika ya wapiganaji wanapokuwa vitani katika enzi za vita vikali.

photo