audio
“Tumbiri Mzee” Kazi ya Takamura Koun (Roen)
Sanaa za Kijapani
dk13 sek35

Siku ya kutangaza Novemba 19, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Mchongo wa tumbiri kwa kutumia mbao ulichongwa mwishoni mwa karne ya 19. Akionekana akiwa ameketi kwenye jiwe huku mwili wake ukionekana dhahiri kwamba umegeuka upande wa kulia, na kukodoa macho upande wa juu huku akiwa ameshika manyoya mkono wake wa kushoto. Alikuwa akipambana na tai lakini ndege huyo akafanikiwa kutoroka. Sanamu hiyo ina unganisha nguvu isiyo ya kawaida na usahihi wa kazi. Hata manyoya yanayofunika mwili wake yamechongwa tofauti katika kila sehemu ya mwili. Sanamu hiyo ina urefu na upana wa zaidi ya mita moja na unene wa sentimita 76. Sanamu hii ilitengenezwa na Takamura Koun, mchongaji wa sanamu za kibuddha, ambaye alishiriki maonyesho ya dunia yaliyofanyika Chicago mwaka 1893. Mara nyingi wachongaji wa Kijapaji walikuwa wakitengeneza sanamu za kibuddha kwa kutumia mbao kama nyenzo. Tumbiri huyu ni kazi iliyowakilisha Japani katika kipindi ambapo Japani ilikua inaanza kugundua kuhusu sanamu kubwa zenye uhalisia kutoka magharibi na sanamu za Kijapani zilkuwa zimeanza kubadilika.

photo