audio
Ramani ya Japani iliyochorwa na Ino Tadataka (Nihon enkai yochizu)
Sanaa za Kijapani
dk16 sek08

Siku ya kutangaza Oktoba 15, 2015
Inapatikana hadi Machi 31, 2029

Nihon Enkaiyochizu – Ramani za Japani zilizochorwa na Ino Tadataka – zilitengenezwa mapema katika karne ya kumi na tisa. Zikiwa na usahihi wa hali ya juu na kuchorwa kwa njia ya picha nzuri, ramani hizo zilitumia rangi zisizokoza za kijani, buluu na rangi nyingine na ule ujumuishaji wa pamoja wa ramani ulitolewa na mistari mekundu iliyokuwa ikiweka rekodi ya utafiti wenyewe. Ino Tadataka alisafiri kwa miguu kote nchini Japani kwa miaka kumi na saba akianzia akiwa na umri wa miaka hamsini na tano. Usahihi wa ramani zake pia unatokana na ukweli kwamba, yeye alikuwa ni mtafiti wa kwanza nchini Japani kuweza kuchanganya vipimo ardhini na mwenendo wa sayari mbinguni. Ino alianza kazi hiyo kama raia binafsi lakini alikuja kuaminiwa na serikali ya Shogun na hatimae kazi yake kugeuka kuwa mradi wa taifa. Ramani zake baadaye zilitumika kwa miaka mingi kama msingi kwa ajili ya ramani zilizotengenezwa kwa mbinu za kisasa za utafiti.

photo